Thursday, January 14, 2010

Ligi Kuu ya Vodacom

Mechi za Dar live kupitia ITV
Kituo cha luninga cha ITV kitarusha moja kwa moja mechi zote za ligi kuu ya Vodacom zitakazopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

Ligi hiyo iliyokuwa imesimama baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza, inatarajiwa kuendelea Jumamosi ijayo pamoja na michezo mingine, Yanga itajitupa kwenye Uwanja wa Uhuru kupambana na African Lyon

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, ITV inatarajiwa kurusha matangazo hayo sambamba na kituo chake cha redio - Radio One Stereo.

Katika raundi ya pili, Yanga ina mchezo mmoja tu nje ya Dar es Salaam dhidi ya Prisons ya Mbeya.

1 comment:

MASEBE said...

VIPI MBONA MECHI YA MNYAMA HAIKURUSHWA? ZINARUSHWA MECHI ZA TIMU YA WANANCHI PEKE YAKE AU. TUNAOMBA MWONGOZO.