Saturday, January 16, 2010

Ligi Kuu ya Vodacom

Yanga vs African Lyon
Mzungukao wa pili wa ligi kuu ya Vodacom inatarajiwa kuanza leo kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Yanga itakapopambana na African Lyon.

Yanga inaanza mzunguko huo ikiwa katika nafasi ya tatu, nyuma ya timu za Simba na Azam. Simba ina pointi 33 wakati Azam ina pointi 21 sawa na Yanga lakini ina faida ya kuwa na magoli mengi ya kufunga.

African Lyon imejiimarisha katika dirisha dogo la usajili baada ya kuwaongeza wachezaji wazoefu kama Ivo Mapunda, Meshack Abel, Geogre Nyanda, Adam Kingwande na Vincent Barnabas. Pia benchi lake la ufundi limeimarishwa kwa kumkabidhi Charles Boniface Mkwasa mikoba ya kuinoa timu hiyo.

Yanga inatarajiwa kuendeleza makali yake iliyoonyesha katika kombe la Tusker, hivyo pambano hilo linatarajiwa kuwa la kuvutia.

29 comments:

Anonymous said...

Nawatakia kila la kheri ktk mzunguko wa pili mpira wa kitabuni kama yunavyoona ktk magazeti na ushindi ikiwezekana mzunguko wote bila kupoteza mtupe habari kama kawaida hatupo nyumbani daima mbele nyuma mwiko yanga damu baghdad

Anonymous said...

vipi huko

CM said...

dakika 36 bado 0-0

CM said...

tumepata bao la kwanza ktk dk ya 44 kupitia kwa Jerry Tegete

CM said...

Halftime
Yanga 1 African Lyon 0

Anonymous said...

mpira bado haijaisha

Anonymous said...

cm mambo vipi vijana wa papic wanaupiga? mdau italy

CM said...

dakika 90 zimemalizika kwa ushindi wa mabao 2-0

Tegete (44) na Ngassa (90)

Anonymous said...

Asante CM, nadhani ushindi huu utatupa moto wa kusonga mbele! Naona wachezaji wazawa wanazidi kumuonesha Kondic kwamba falsafa yake ya kujaza wachezaji wa kigeni yanga haikuwa na manufaa kwa club kwani hawajaonesha mchango wao msimu huu, hasa katika kucheka na Nyavu!
Mdau, ughaibuni!

Anonymous said...

hebu tupe tathmini kamili ya mchezo

Anonymous said...

alafu na msimamo ukoje?

Anonymous said...

Mnyama kapiga mtu tena, haya majamaa yatachukua Ubingwa mapema tu.

Anonymous said...

kakupiga wewe acha umbeya

Anonymous said...

jamani jinyama vipi mlio nyumbani?

mdau italy

Anonymous said...

Mnyama kashinda goli 2, magoli yote yamefungwa na Mgosi, jamaa wakishinda mechi nne tu, watakuwa wamechukua Ubingwa

Anonymous said...

mwaka huu ni wao sisi tujipange mwakani

Anonymous said...

mnakumbuka shuka kumeshapambazuka hahahaha

Anonymous said...

kamwambie mkeo,hahahahahahahahaha

MOJAONE said...

vipi mechi ya leo ya simba inaendeleaje?

Anonymous said...

mnyama anaongoza 2-0
mgosi na nyagawa

Tina said...

haya mnyama katafuna tena leo
Simba 2 Vs Prisons 1

Mgosi x 2
Nyagawa

Anonymous said...

samahani simba 3 Prisons 1

Anonymous said...

nafikiri wazo busara mnyama si mwenzetu mwaka huu tujifue mabingwa wa africa kwani speed ya mnyama kali mnyonge mnyongeni haki mpeni ubingwa wake .


jangwani halisi.

MOJAONE said...

Wahusika wa hii web mko wapi habari zote za zamani, hakuna mtu ana update kabisa yaani habari za Yanga tunazisoma kungine kabisa wakati zilikua zitoke hapa kwanza na ndio vyombo vingine vinukuu, kama mmeshindwa kazi tupeni sisi hiyo password tu-take care for this website. Nawashukuru waungwana mliopo Bongo kwa ku update na kutupa matokeo za mechi moja kwa moja endeleeni pia leo kutupasha..

MOJAONE said...

Washkaji msitusahau basi matokeo ya Yanga na manyema leo hii tupeni matokeo kila wakati, maana wahusika wa web hii wamelala!!!

MOJAONE said...

Mechi imeshaanza au bado wanajangwani??

Anonymous said...

Mechi bado saana, sasa hivi ni saa tisa mchana

MOJAONE said...

Sawa msitusahau tu.

MOJAONE said...

mambo yanasemaje huko??