Yanga vs Majimaji
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Voodacom, Yanga leo wanajitupa katika Uwanja wa Uhuru kupambana na Majimaji ya Songea katika mchezo wa ligi hiyo.
Yanga bado wapo katika mbio za kutetea taji lake licha ya kuachwa pointi 12 na mpinzani wake mkubwa Simba ambao leo watakuwa huko Mwanza kupambana na Toto Africa ya huko.
Katika mchezo wa leo, Yanga itawakosa wachezaji wake Mrsho Ngassa (mgonjwa), Kabongo Honore(majeruhi) na Nurdin Bakari (kadi tatu za njano). Kwa hali hiyo huenda mchezaji wa kimataifa kutoka Uganda Steven Bengo akachezeshwa katika pambano la leo.
Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizi mbili uliopigwa huko Songea, Yanga ililala 1-0.
19 comments:
list ya leo:
1. Obren
2. Nsajigwa
3. Maftah
4. Wisdom
5. Nadir
6. Bonny
7. Shamte
8. Chuji
9. Tegete
10. Ambani
11. Kiggi
dk. 21 Yanga 1 Majimaji 0
Boniface Ambani
asante sana cm mwendo mdundo
italy
HT 1-0
mechi ya Simba na Toto Africa itachezwa kesho
nawatakia kila la kheri wana yanga wote mwendo mdundo hakijaanza kipindi cha pili kuwait ?
matokeo bado moja bila
YANGA WAMEPATA GOLI LA PILI DK YA 19 KIPINDI CHA PILI LIMEFUNGWA NA AMBANI TENA
dk 68 Ambani amefunga mabao mawili ya haraka.
Tunaongoza 3-0. Ambani's hattrick
bado yapo magoli
naona ambani karudi ktk fomu
dk 80 Yanga down to ten men, Wisdom Ndhlovu sent off for second bookable offence.
dakika 90 zimemalizika kwa ushindi wa 3-0
Yanga sasa imefikisha pointi 30 ikiwa ni pointi 9 nyuma ya Simba ambayo itacheza kesho na Toto Africa.
asante saana wana jangwani asnte cm
papo kwa papo kamba hukata jiwe
italy
jamani vipi jinyama limelala kwa wanetu toto? naliombea dua mbaya lidode,
No, mnyama kashinda 3 -1, habari ndiyo hiyo, labda tungoje kwa Kagera Sugar sasa.
Hapana, mpira bado unaendelea matokeo ni kwamba Simba 0, Toto 0
FULL TIME CCM Kirumba Mwanza Simba 2 Toto Africa 0
Mgosi dk 52, Redondo dk 54
hahaha dua yako imeota mbawa.mkubali mwaka huu hampati kitu.mnyama mkali tuu.ubingwa unatua msimbazi.oh kidedea.
Post a Comment