Saturday, February 27, 2010

Ligi ya Mabingwa Afrika

Lupopo vs Yanga
Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga leo inapeperusha bendera ya taifa huko Lumbumbashi DRC wakati itakapopambana na FC Lupopo ya huko kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Stade de Kenya jijini Lubumbashi.
Habari za hivi punde kutoka huko Lubumbashi zinaeleza kwamba Yanga imefanya mabadiliko ya kikosi chake kilichoanza katika mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita ambapo Kipa atakaa Obren Circkovic wakati George Owino atacheza beki namba nne huku Godfrey Bonny na Jerry Tegete wakianza.
List kamili:
1. Obren
2. Nsajigwa
3. Maftah
4. Owino
5. Nadir
6. Chuji.
7. Nurdin
8. Bonny
9. Tegete
10. Ngassa
11. Kiggi
Yanga inahitaji ushindi wa mabao 2-0 ili isonge mbele kwenye michuano hiyo. Pambano hilo linatarajiwa kuanza saa kumi na nusu kwa saa za Afrika Mashariki.

23 comments:

Anonymous said...

half time tunaongoza 1-0.goli kafunga tegete.tunacheza vizuri.ushindi upo.

Anonymous said...

cm kaka tuko mbali huku toa rada za kweli maana humu wanyama kibao

Anonymous said...

mpira umeanza saa 11 hivi iwe halftime sasa tunaongopeana

Anonymous said...

cm vipi matokeo bado haujapata?

Anonymous said...

cm hata kama tumelambwa toa rada kaka wengine tuko mbali na bongo wewe ndio luninga wetu

Anonymous said...

jamaa wamesawazisha.1-1

Anonymous said...

Bado matokeo ni 1-0 mdau hapo juu wewe Simba nini?

tina said...

tupeni matokeo ya ukweli jamani.

Anonymous said...

Mechi inatangazwa live kwenye linki hii kama kifaransa kinapanda... http://www.surfmusic.de/radio-station/radio-okapi,5147.html

Anonymous said...

Ni dakika ya 48 kipindi cha pili, tuko mbele kwa 2-1, tunahitaji tofauti ya magoli 2 ili tusonge mbele

Unknown said...

Mwanangu Tegete anapiga bao la 3 dakika 62, sasa ni 3-1

Anonymous said...

Mwanangu Tegete anapiga bao la 3 dakika 62, sasa ni 3-1

Anonymous said...

Nasikiliza kifaransa lakini sielewi. TBC hawangazi kwani CM?

CM said...

Mpira hautangazwi na kituo chochote hapa TZ.

Tunashukuru kwa mdau huyo aliyetoa link ya Radio Okapi - Kinshasa ambao wanatangaza game hiyo kwa Kifaransa

Anonymous said...

duh CM nalia hapa kifaransa haklpandi naona maluweluwe tuu-SGM
Hakuna radio inatoa updates huko kwani ngapingapi sasa-SGM

Anonymous said...

Duh noma tumetolewa Lupopo watacheza na Dynamo ya Zimbambwe round inayofuata hata hivyo tumejitahidi sana

Unknown said...

matokeo?

Anonymous said...

cm toa mziki

Anonymous said...

SGM na wadau wengine vuta subira kidogo tunasubiri kipindi cha michezo kitaanza saa 1 kamili ya huku

CM said...

Yanga imetolewa katika michuano ya Klabu bingwa baada ya kufungwa 1-0 leo.

Anonymous said...

Jamani tumeyaaga? naona kimya sana.

Anonymous said...

sasa mbona webmaster unaacha watu kuweka matokeo ya uwöngo humu.nilikubali tumeshnda.ah yanga aibu tupu

Unknown said...

Kama inawezekana webmaster fanya uchambuzi kabla comment haijawa published, ni kweli wote tuna akili timamu lakini tunatofautiana kwa uwezo wa kupambanua na kustahimili vitu. Angalia comments zenye uchochezi wa aina yeyote usizitoe kwani wengine wana hasira za karibu na ndio tunaona matusi ndani ya blog yetu. Tumesema hii ni blog ya wanachama na wapenzi wa yanga, hivyo wewe kama si mmoja wao soma na kisha acha. Tunapokea ushauri wenye kujenga lakini sio kebehi.