Tuesday, April 06, 2010

Tegete atarudi Ulaya?
Dili la mshambulijaji wa Yanga Jerry Tegete kucheza soka la kulipwa huko Sweden, limeota mbawa baada ya klabu yake kumtaka arejee nchini licha ya kufaulu majaribio.

Tegete ambaye aliondoka nchini Machi 18 mwaka huu, alitua katika klabu ya Dalkurd FF ya Sweden kufanyiwa majaribio ambayo alifaulu na klabu hiyo kumtaka ajiunge na nayo kwa mkopo wa miezi mitatu.

Awali wakala wa mchezaji huyo Bw. Damas Ndumbaro alitoa taarifa kwamba mchezaji huyo atarejea baada ya wiki mbili lakini wakati wiki mbili zikikaribia kumalizika, Ndumbaro aliiarifu Yanga kwamba mchezaji huyo amefaulu majaribio na klabu hiyo inaomba abaki huko Sweden ili ajiunge na Dalkurd FF kwa mkopo wa miezi mitatu.

Baada ya taarifa hiyo, klabu ya Yanga ilikataa ofa hiyo na kumtaka mchezaji huyo arejee nchini ili mazungumzo yafanyike. Yanga inadai kwamba makubaliano yalikuwa ni majaribio ya wiki mbili kisha mchezaji huyo arejee nchini kuitumikia klabu yake katika mechi mbili zilizosalia za ligi kuu ya Vodacom.

Hata hivyo tayari Ndumbaro alikaririwa na redio moja nchini akisema kwamba dili hilo la Tegete limekufa na mchezaji huyo atarejea nchini katikati ya wiki.

Mapema mwaka jana mchezaji mwingine Mrisho Ngassa aliwekewa ngumu na uongozi wa klabu hiyo baada ya wakala wa mchezaji huyo kumtafutia timu huko Norway - Lovham FC lakini Yanga ikataka taratibu zifuatwe.

Pia katikati ya miaka ya 90 mchezaji Edibiliy Lunyamila alirejeshwa nchini kutoka kwenye majaribio huko Ujerumani ili aikabili Simba katika mechi ya ligi. Baada ya mechi hiyo Lunyamila hakubahatika tena kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

8 comments:

Anonymous said...

Hizo habari ni za ukweli? lakini kama waliomba kibali cha wiki 2 hizo za miezi 3 ya mkopo wamepitishiana na nani? ni vizuri maslahi ya mchezaji na club yakaangaliwa

Paul Akwilini said...

Mchangiaji wa hapo juu naungana na wewe. kwa maana mi ninavyojua ni kwamba kama kuna timu inamuhitaji mchezaji, hukaa chini na clabu husika na kufanya mazungumzo nayo. ulaya wanaita dil

Anonymous said...

klabu za ulaya ndizo zilivyo,wanafikiri waafrika wanaashida sana nchi zao.sioni kosa la yanga kwa sababu wamejifunza na kosa la nadir .tegete usiwe na homa ndugu ile ilikua dili ya ubabaishaji tuu.

Anonymous said...

sasa kama waliomba kibali cha wiki mbili na wakaona kuwa anafaa wakaomba cha miezi mitatu sasa tatizo liko wapi?? mi sioni tatizo hapo ila tatizo liko kwa Yanga hali hii ya kuwawekea wachezaji ngumu sio nzuri hata kidogo kwani ni wakati wakuangalia maslahi ya Mchezaji kwanza kwani kama kuitumikia timu keshaitumia vya kutosha ni wakati wake wa kuimarisha maisha yake kwani umri hamusubiri. Jamani Yanga tuamke!!

Anonymous said...

Kwanza nashukuru mdau kutuwekea blogu hii maana chama letu sijuwi nimeshikwa nanini linashindwa weka blogu yetu mtandaoni...? kuhusu wachezaji kurudishwa pindi wanapokwenda majaribioni mimi naungana na klabu... kwa taarifa yetu hapo kuna kono la mtani ili kutozoofisha kwenye game lijalo washindwe na walegee.. mfano miaka ya nyuma Athumani Abdallah China aliondoka kwa mtindo huu.. karibu na mechi na alitudi mechi imeshapigwa na ili kutufumba macho wakampiga hogo(POP) la mkono ili tujue ni mgonjwa kumbe ili kuwa mbinu yao... kwa Tegete wameshindwa... Huyu Ndumbalo nani asiye mjua kwamba Mnyama damu... lazima wang'oke tu...

Anonymous said...

tukitaka maendeleo ya kweli ktk soka lazima tuache mawazo duni ya yanga na simba,mechi ya simba na yanga ya j2 aina jipya ,simba bingwa tayari na yanga ni ya 2,ni kama mechi ya kukamilisha ratiba tu,viongozi tumieni busara kijana ajitafutie maisha soka ndo kazi yake,tazama kambi ya mechi na simba tumeweka sehemu bora holiday inn ,hii ilipaswa tufanye wakati wa mechi ya lupopo ambayo kisoka ilikua muhimu zaidi ya hii ya j2,kwa mpango huu kila mwaka tutaishia pua chini.

Anonymous said...

[url=http://louboutinmart.co.uk]christian louboutin outlet uk[/url] Ms. http://dkgoose.com Icluwatmn [url=http://csrhelix.com]Canada goose outlet [/url]
fdroke 520656 [url=http://www.chilliwackbombersoutlet.com]mens canada goose jacket[/url] 551260 [url=http://www.officialcanadagooseparkas.ca]canada goose in toronto[/url]

Anonymous said...

[url=http://louboutinmart.co.uk]louboutin uk[/url] Synthetic supplements or libido boosters work by vigorously changing your physiology and which makes it what you want so that it is instead of permitting it to induce exactly the same effects by itself terms. [url=http://dkgoose.com]Canada Goose Parka[/url] Ildrmlqpu [url=http://www.louboutinoutletuks.co.uk]christian louboutin uk[/url]
kgchgg 682497 [url=http://www.chilliwackbombersoutlet.com]canada goose down vest[/url] 218686 [url=http://www.beatsbydreaonsales.com]beats by dre christmas[/url]