Wednesday, April 21, 2010

Yanga kuishusha Prisons leo?

VILIO au vicheko vitakavyotawala leo katika majiji ya Mwanza na Mbeya baada ya filimbi ya mwisho kupulizwa wakati timu za Toto African na Prisons zitapotupa karatazao za mwisho za kubaki Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara kwa msimu mwingine.

Mechi nyingi za leo zinachukuliwa kama za kukamilisha ratiba ya ligi kwa timu nyingi isipokuwa kwa Toto African, Prisons na Manyema ambapo ni klabu moja tu inayoweza kujinasua kutoka kwenye janga la kushuka daraja msimu huu baada ya Moro United kuaga mapema.

Maafande wa Prisons na Toto African wote wana jumla ya Pointi 20 kila mmoja huku Manyema Rangers ikiwa juu yao kwa tofauti ya pointi mbili zaidi. Manyema wenye kibarua kizito dhidi ya Azam watakuwa wakiomba Prisons na Toto zipoteze mechi zao ili ibaki kwenye ligi.

Prisons ikishinda itafikisha pointi 23 na itakuwa mbele ya Manyema yenye pointi 22 na Toto African pointi 20,hivyo Manyema na Toto kuungana na Moro yenye pointi 15 kushuka daraja.
Prisons watakuwa kwenye uwanja wa Sokoine kuikabili Yanga. Wakati Toto watakuwa ugenini mjini Bukoba kwenye Uwanja wa Kaitaba kuwakabili wenyeji Kagera Sugar wenye pointi 23 ambao matokeo mabaya ya mchezo huo yanaweza kuwashusha daraja.

Endapo timu hizi tatu za mwisho zote zikishinda kwenye michezo yao Toto itafikisha pointi 23 kama Prisons ikishinda, lakini Manyema Rangers watanusurika kushuka daraja kwa kufikisha pointi 25.

Lakini hali hiyo inaweza kuchukua sura mpya kama Toto wataiifunga Kagera Sugar, Manyema wakatoka suluhu na Azam, huku Prisons wakiichapa Yanga mabao mawili timu zote nne za mwisho zitafikisha pointi 23.

Kwa kuwa Toto imeshafunga mabao 23, Manyema 20, Prisons 18 wakati Kagera imeziona nyavu mara 14 tu.

Hapo ndipo Kagera Sugar na Manyema Rangers zitakapoungana na Moro United kushuka daraja kwa kutumia sheria ya mabao mengi ya kushinda katika kuamua.
MSIMAMO WA LIGI MSIMU WA 2009/10

21 comments:

CM said...

haltime Mbeya, bado 0-0

Anonymous said...

Vipi mnyama rekodi yake imetubiliwa leo au vipi

Anonymous said...

inakuhusu nini wewe umeshatandikwa kaa kimya.

CM said...

Mnyama mambo yake mazuri anaongoza 4-0. Huu ni mwaka wao

CM said...

Prisons 1 Yanga 0

Anonymous said...

Wewe unayeuliza matokeo ya Simba utachoka bure.Mwaka wa Simba huu.

CM said...

Dk 85 Prisons 1 Yanga 1 Steven Bengo

CM said...

Full time:
Prisons 1 Yanga 1
Mtibwa 0 Simba 4
Toto 3 Kagera 1
Lyon 1 JKT 0
Manyema 0 Azam 0
Majimaji 0 Moro 2

Moro, Prisons & Manyema relegated

Anonymous said...

Fukuza timu nzima jangwani.mamilioni tumesajili wachezaji na hakuna matunda.hongera mnyama mwaka huu ni wenu mesajili timu kali, wachezaji kama haruna moshi na mrwanda wamepata timu nje ya nchi na ligi meshina bila mastaa hao wawili.well done.yanga wachezaji mabangi tuu na hata mchezaji moja hajapata timu kucheza soka ya kulipwa

tina said...

na mgosi ndiye mfungaji bora.oh kidedea.

Anonymous said...

sikio la kufa alisikii dawa,tayari yanga imesajiri mizigo mingine bomu toka ghana kwa mamilioni ya dola,mwakani msubili kichapo tena,kaaaaaziiii kweli yeboyebo.

Anonymous said...

Sijui mtajifunza lini kuwa hao mabomu mnaowasajili ni watalii tuu na wanakuja kuwanyoa mifukoni.kama kweli ni mastaa mbona wanaonekana kwa yeboyebo tuu na siyo timu zingine.kweli mtabakia kutia aibu.nyota wamejaa tanzania ila basi mnajifanya eti klabu tajiri katika kanda.meona mastar waliyosajiliwa msimbazimnendeni mkamkatieni rufaa tena uhuru selemani.mtabaki wajinga tuu

Anonymous said...

Na bado mwakani lazima wagalagazwe tu pamoja na mamilioni yao!!!

Anonymous said...

wataalamu naomba tathmini yenu kuhusu timu yetu msimu huu tatizo lilikuwa ni nini? tulitumia pesa nyingi kusajili kuliko timu yeyote na hao maprof baadae waliishia kuwa watazamani tu, je tumejifunza nini? tatizo ki kocha au wachezaji?

Anonymous said...

Hivi mamilioni ya Yanga inaelekea Simba yanawauma kweli! Naona kila siku mamilioni ya Yanga tuu. Kama nyie hamna pesa si mnyamaze tuu. Mbona mnakuwa kama 'wakuja'????

Anonymous said...

Sisi mambo yetu tunayafanya uwanjani na sio kwenye mabenki. Tunawatakia mambo mema na mamilioni yenu wakati sisi tunachukua vikombe.

Anonymous said...

Vikombe gani hivyo ambavyo Yanga haijawahi chukua?

Anonymous said...

acha kulumbana na wanasimba hatuwawezi ,yule mkiti wao kumbe hana ata elimu ya kuiongoza klabu alikua anaongoza kininja tuu.

Anonymous said...

mpira uwanjani siyo kwenye mtandao. kuweni wastaarabu kwa kukubali mwaka huu ni wa mnyama. mechi zote mbili kawalamba na ubingwa kachikua bila ya kupoteza mchezo wowote. mnataka nini zaidi ya hayo??? Yebiyebo kubalini tu! Mwenzenu mwarabu leo kaonja shubiri!!!! nyie endeleeni kucheza mpira mtandaoni na kwenye ATM

Anonymous said...

Hayo ya mwarabu zungumza baada ya mechi ya marudiona siyo sasa hivi.

Anonymous said...

Afadhali Simba analinda heshima ya nyumbani nyie mlitundikwa na timu mbovu ya Lupopo nyumbani na ugenini.Lupopo ambaye ni nyanya kafungwa na Dynamos nyumbani na ugenini.Mnashindwa hata kushinda nyumbani mnabaki na mpira wa magazetini na kujidai utajiri.Mpira uwanjani sio mdomo migongo wazi.