Saturday, July 24, 2010

Salva kocha msaidizi Jangwani
KLABU ya Yanga imemteua nahodha wa zamani wa timu hiyo Salvatory Edward kuwa kocha msaidizi kushirikiana na kocha mkuu Mserbia Kostadin Papic.

Pia aliyekuwa Meneja wa timu hiyo Kenneth Mkapa, sasa atakuwa kocha wa kikosi cha pili cha timu hiyo.

Uteuzi wa Salvatory unafuatia maombi ya kocha huyo kutafutiwa msaidizi ambaye hajawahi kuwa kocha katika timu yoyote hapa nyumbani.

Nafasi ya meneja wa timu itazibwa kwa muda na Emmanuel Mpangala.

1 comment:

Gray said...

Kwa kweli natoa pongezi kwa uteuzi wa kocha msaidizi. ni wazi kuwa sasa Yanga tutakuwa imara kwani kuwa na kocha mmoja ilikuwa inazidisha mzigo kwa kocha papic.

pamoja na pongezi hizo nashindwa kuelewa sababu za Mpangala kuendelea kuwemo kwenye benchi la ufundi. kwa ujumla Mpangala hafai. Yanga wote tunajua kuwa Mpangala ni mmoja wa watu ambao wamekuwa na majungu na wachezaji wengi. hata hivyo akiwa katibu wa mashindano ambaye anasimamia ratiba nzima ya mashindano alishindwa kutoa ushauri kwa Uongozi wa juu kuhusu ratiba ya mechi za Yanga msimu uliopita.Ilitulazimu Yanga kucheza Songea jumamosi na J4 tucheze Dar ilihali anajua miundombinu ya nchi yetu. na TFF wakasema kuwa Yanga waliafiki ratiba iliyotolewa na TFF na Mpangala ndiye aliyesaini TFF kuunga mkono ratiba hiyo. MPANGALA HAFAI. Kama ni lazima awepo Yanga mtafutieni kazi nyingine. hiyo kwa msimu huu NO.