Wednesday, January 05, 2011

Minziro kocha msaidizi Yanga

Kocha wa Ruvu Shooting, Freddy Minziro ameteuliwa kuchukua nafasi ya Salvatory Edward kuwa msaidizi wa Kostadin Papic Yanga.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilizopatikana Dar es Salaam jana zilisema kuwa tayari Yanga imesharidhiana na uongozi wa Ruvu Shooting, hivyo Minziro anatarajiwa kuungana na Yanga leo Zanzibar.

“Ndio hivyo, ni kweli taarifa hizo zipo kwamba Minziro sasa anakuwa msaidizi wa Papic Yanga baada ya kuonekana nafasi ya usaidizi Salva haimudu ndio maana uongozi ukaona umpe jukumu hilo Minziro,” alisema mtoa habari wetu ndani ya Yanga.

Hata hivyo huenda hiyo ndio safari ya Minziro kupewa Yanga kwani kocha Papic mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu na kuna kila dalili za kutohitajiana, si Yanga wala Papic anayemhitaji mwenzake.

Habari zilizopatikana jijini juzi zilisema kuwa kocha huyo tayari ameshaanza kufanya mchakato wa kutafuta nyingine ya kufundisha atakapoondoka Yanga na ameagiza rafiki zake sehemu mbalimbali kumfanyia kazi hiyo.

Inadaiwa kuwa kinachomfanya Papic aondoke ni hali ya kukosekana kwa morali kwa wachezaji ambao hivi karibuni waligoma wakishinikiza kulipwa sehemu ya fedha zao za usajili.

“Kocha amechoshwa, anahisi timu itafanya vibaya kwenye mashindano kwa vile wachezaji hawana morali kutokana na kudai fedha zao za usajili, pia klabu haina fedha kwa sasa kwani mfadhili wetu Yusuf Manji ni kama hayupo kwa vile hatoi tena msaada kama ilivyokuwa mwanzo na kusababisha klabu kushindwa kujiendesha”.

31 comments:

Anonymous said...

pole mr minziro ,lakini karibu.

Anonymous said...

Ndio maana soka la bongo haliendelei. Yaani makocha ni walewale miaka nenda miaka rudi. Minziro ana lipi jipya? Kama ni hivyo basi mpelekeni japo Ulaya akapate mafunzo

Anonymous said...

bahili hawa watafanya nini?eti tunajilinganisha na tp mazembe,bajeti yao ya mwezi ni sawa na yanga miaka mitano ,bisha basi.

Anonymous said...

sasa imekuaje mchezo wa yanga na azam?

Anonymous said...

yang 2 azam 1..magoli yamefungwa na nsa job na idd mbaga.
yanga na ocen view wamaingia nusu

Anonymous said...

asante sana ,tafadhali unaweza kupost habari yoyote ya yanga pindi upatavyo au ya taifa stars mimi nakua na shauku kubwa kuangalia matokeo ,ntakushukuru sana .

Anonymous said...

Leo vipi nani kalal kati ya yanga na Mtibwa?

Anonymous said...

mtibwa kapigwa 2 - 1 bado mnyama. lazima achinjwe

Anonymous said...

wafungaji nani?

Anonymous said...

Jamani vipi fainali leo,mbona kimya humu.tupatie data ya mechi na mikakati jamani

Anonymous said...

Fuatilia kwenye website ya Yanga. www.yangasc.com

Anonymous said...

simba 1 sie 0, half time

Anonymous said...

Simba 2 - Yebo Yebo 0

Anonymous said...

huna adabu hata kidogo ,kwanza hakuna umeme ulipo.

Anonymous said...

Utajiju! Habari ndio hiyo. Mnyama kashapiga viwili sasa kazi kwenu.

Anonymous said...

simba 2 yeboyebo 0 gori la pili limefungwa mkina dk 62, go www.yangasc.com

Anonymous said...

DK 61: Simba wanapata goli la pili. Mfungaji Shija Mkina. Makosa ya walinzi wa Yanga.

DK 58: Kona kwa upande wa Yanga. Simba wanaokoa

DK 56: Yanga wanapata faulo. Simba wanaokoa unakuwa wa kurusha

DK 52: Godfrey Bonny anatoka anaingia Insa Job

DK 50: Isack Boakye anakosea lakini Mgosi anakuwa sio makini. Nafasi ya wazi kwa simba

Dk 48: Ochan anakosa goli, Yaw Berko anaokoa

Dk 47: Mgosi anaonyeshwa kadi ya Njano

Mpira umeanza kipindi cha pili

Anonymous said...

Visingizio vimeanza hah! hah! hah!

Si rahisi Yanga warudishe haya magoli. Wanaonekana ku-panic

Yanga ina wachezaji watatu tu waliocheza mechi ya ligi dhidi ya Simba kule Mwanza na kushinda. Simba inawakosa wachezaji watatu tu Nyoso, Kaseja na Yondani

Anonymous said...

yes hayo ndio mambo sio wewe unawaita hao yebo yebo kwani hujafundishwa adabu?

Anonymous said...

hah! hah! hah! sasa unakataa Yanga sio yeboyebo?

Anonymous said...

wewe na family yako yebo yebo.

Anonymous said...

hah! hah! hah! na bado mwaka huu yeboyebo mdebwedo. Yaani mtakata viuno kwa kwenda mbele wakati Mnyama anajinafasi!!!

Anonymous said...

nilisahau kumbe wewe punguani ,samahani kwaheri.

Anonymous said...

Mwali kapata Mume leo, Mnyama kafanya kweli. YeboYebo chaliiiii!!!!!

Anonymous said...

wape nyuma basi myama

Anonymous said...

Mpira umekwisha Yanga 0 - Simba 2..

Anonymous said...

Labda m**a yako ndio atoe!! mtalijua jiji mwaka huu!! yeboyebo mdebwedo

Anonymous said...

Yaani pamoja na million hamsini za manji Mnyama kachukua mwali!! sio mchezo!!

Anonymous said...

2 kavu bila mate leo, duuh sipati jibu maumivu ya makalio ya ma miss wa jangwani ila mmeshazoea nyinyi,another MBA lenu MWAPE ajapiga hata kishot kimoja mmeliwa tena.

Anonymous said...

neno jipla la kiswahili-YANGA-maana yake ni kutofika kwa mtu au watu kwenye sehemu au kazi kwa wakati unaotakiwa au muda uliopangiwa.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___