Monday, January 24, 2011

Mwalusako ajiuzulu Yanga
Katibu Mkuu Lawrance Mwalusako kujiudhuru kwa sababu alizoziita za "kiafya".

Juzi Mwalusako aliandika barua kwa mwenyekiti Nchunga ya kujiuzulu kuendelea kuitumikia klabu hiyo akiwa kama katibu wa kuajiliwa.

Habari za uhakika zilizotolewa na mmoja wa viongozi wa Yanga zimeeleza kuwa Mwalusako kajiuzulu baada ya kukutana na Manji na kumtaka afanye hivyo kwa sababu hataki kufuata anayoagizwa na mdhamini huyo.

Kiongozi huyo alisema mdhamini huyo alichukizwa na Mwalusako kwenda kwenye mkutano wa viongozi wa Matawi ambao ulimtaka Nchunga asimamishwe kutokana na kutaka kuiuza Yanga kinyemela bila kushirikisha kamati ya Utendaji.

Alisema kosa jingine lililomtoa Mwalusako ni kuikana barua ambayo ilikuwa imeandikwa na Nchunga kwa Francis Kifukwe ya kumtaka atafute watu kumi watakatoa milioni 50 kwa Mwaka na kufikisha milioni 500 ambazo zitakuwa kama mtaji wa kuanzisha Yanga Kampuni.

Mbali na hayo pia Manji alimwambia kuwa astahili kubaki Yanga kutokana na ubadilifu wa fedha alioufanya ambazo zilikuwa ni fedha za usajili 100 milioni ambazo Mwalusako alishazitolea ufafanuzi.

Kiongozi huyo alidai kuwa Manji amekuwa akitumia fedha zake kwa ajili ya kuwapa wanachama kitu kidogo na kuendeleza migogoro inayoendelea hivi sasa.

Source - Mwananchi

1 comment:

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___