Saturday, February 05, 2011

Ligi Kuu ya Vodacom

Majimaji vs Yanga leo
BAADA ya kuadhibiwa na Mtibwa kwa bao 1-0, Yanga leo inatakuwa ugenini mjini Songea kuikabili Majimaji katika mpambano utakaofanyika kwenye Uwanja wa Majimaji.

Kikosi cha Yanga ambacho kiliondoka jijini Dar es Salaam juzi mchana kikiwa na wachezaji 20, tayari kimewasili mjini hapa. Awali walishindwa kufika hapa kwa wakati baada ya basi wanalolitumia kusafiria kuharibika maeneo ya Chalinze mkoani Pwani.

Yanga ambayo bado inashikilia usukani wa ligi hiyo kwa pointi moja, 31 huku Simba ikiwa na pointi 30, itabidi ifanye kazi ya ziada kuchukua pointi tatu mbele ya Majimaji yenye pointi 10 ambayo itapigana kutaka kujinasua kutoka mkiani inakoshikilia nafasi ya 11 kati ya timu 12.

Ugumu mwingine wa mpambano wa leo unatokana na sababu za kihistoria ambazo zinatueleza kuwa vijana hao kutoka Mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es Salaam mara nyingi wamekuwa wakiambulia matokeo mabaya wanapocheza katika dimba hilo la nyumbani la Majimaji.

Kocha wa Yanga, Fred Felix Minziro alisema juzi kabla ya kuondoka kuwa amewaambia wachezaji wake wajiepusha na kufikia matokeo yaliyopita bali wajipange kuhakikisha wanashinda mechi ya leo na nyingine zinazofuata.


6 comments:

Anonymous said...

bado matokeo?

Anonymous said...

tupeni matokeo

Anonymous said...

HAKUNA ANYESIKILIZA JAMANI?

Anonymous said...

ngoma draw.

Yanga 1 Vs Maji Maji 1
Tumekosa penalti dakika 88
tusubire miujiza ya Timbe

CM said...

full time 0-0

Anonymous said...

Yanga wamenapata wanachostahili kabisa. Mpira ni taaluma, taaluma haindani kwa mantiki za mdomo bila kuzingatia utaalamu.
Watu wamekuwa na majibu mepesi kwa matatizo mazito. Jaribu kujiuliza unamwondoa Papic katika kipindi ambacho timu inapaswa kuwa moja na yenye malengo mamoja. Hata neno "timu" tumeshindwa kabisa kujua maana yake na ndio maana twataja majina ya wachezaji tunaowapenda. Kocha mzuri ni yule aliyemjuzi wa anachofundisha na kuweza kuifanya timu ikaunganika na kuleta matokeo yanayotarajiwa.
kwa hiyo ni uendawazimu kumtukana refa kila mara. Minziro anatoa tokeo moja la kukwatuliwa na je alifunga magoli mangapi yakakataliwa na refa.
Uwezo wa minziro ni kufundisha kikocha umiseta na siyo timu itayoifanya yanga iwe ya kimataifa.
Utafundishwaje na kocha aliyekulia mpira wa fitina na aishi bila fitina. Amewahi kuwa kocha wa Yanga je aliweza kuleta matokeo gani?