Friday, March 04, 2011

Yanga vs Simba

Chinja hao!!!!!!!
Hatimaye mpambano unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini, Yanga na Simba zinatarajiwa kupambana vikali kwenye uwanja wa Taifa katika mchezo wa duru la pili la ligi kuu ya Vodacom.

Timu zote mbili zilikuwa zimeikimbia Dar es Salaam, Yanga ikiweka kambi huko Bagamoyo wakati Simba ikivuka maji hadi huko Zanzibar.

Hili litakuwa pambano la kwanza la watani wa jadi kwa kocha Sam Timbe ambaye alianza kuinoa Yanga mwanzoni mwa mwezi uliopita. Silaha kubwa zinazotegemewa na Yanga ni mshambuliaji kutoka Zambia Davies Mwape ambaye alisajiliwa katika dirisha dogo la usajili na ameonyesha uwezo mkubwa katika kupachika mabao. Pia Yanga inajivunia ngome yake ambayo imefungwa mabao manne tu tangu ligi hiyo ilipoanza.

Timbe amekuwa akimchezesha zaidi beki Chacha Marwa na Nadir Haroub tofauti na kocha aliyepita Kostadin Papic ambaye alikuwa akimpa nafasi Issac Boakye kutoka Ghana ambaye tangu alipovurunda katika mechi dhidi ya Dedebit ya Ethiopia, benchi limekuwa likimwandama.

Kwa upande wa Simba nayo pia inajivunia mshambuliaji wake hatari Mbwana Samatta ambaye tangu alipomaliza mgomo wake wa kujiunga na Simba, ameipa uhai mkubwa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Halikadhalika Mganda Patrick Ochan anaonekana 'kufufuka' katika mzunguko wa pili wa ligi.

Katika ulinzi Simba imepata pigo baada ya beki wake Joseph Owino kuumia hivyo nafasi yake huenda ikazibwa na Kelvin Yondani akishirikiana na Juma Nyoso. Katika lango huenda kipa Ally Mustafa 'Barthez' akakaa golini kufuatia kiwango cha Juma Kaseja kushuka katika michezo ya hivi karibuni.

Shughuli nyingine katika pambano hilo inatarajiwa kuwa katika kiungo ambapo Yanga ina wachezaji mahiri kama Godfrey Bonny, Nurdin Bakari, Chuji na Omega Seme huku Simba ikiwategemea zaidi Mohamed Banka, Amri Kiemba na Jerry Santo.

Katika pambano la mzunguko wa ligi hiyo, Yanga iliilaza Simba 1-0 huko Mwanza kwa bao liliofungwa na Jerry Tegete.

Tusubiri dakika 90 za mwamuzi Oden Mbaga.

8 comments:

SHIKABWE MSAFIRI said...

SISI WANA YANGA,TUNAIOMBEA TIMU YETU IWEZE KUSHINDA MCHEZO HUU MUHIMU KWETU.WACHEZAJI WAJIAMINI TU,WALA WASITISHWE NA MTU WATIMIZE WAJIBU WAO USHINDI UPO

Anonymous said...

dk 16 0-0

Anonymous said...

Mtu hajavuliwa chupi mpaka sasa? kwi kwi kwi kwi kwi

Anonymous said...

halftime 0-0

hakuna mashambulizi ya kutisha. Mpira unachezwa zaidi katikati.

Anonymous said...

tunaongoza 1-0

Anonymous said...

tushaanza kufyatuana cm upo wapi? mfungaji nani?

Anonymous said...

1-1

Anonymous said...

mpira bado haujaisha tupeni matokeo nasi tulio nje tujuwe