Sunday, June 26, 2011

KAGAME CUP 2011

Yanga yaanza kwa sare

MABINGWA wa Tanzania Bara, Yanga imeanza michuano ya Kagame 2011 kwa sare ya 2-2 dhidi ya timu ya El Merreikh ya Sudan.

El Merreikh ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya pili lakini Yanga ikarejesha bao hilo dakika nne baadaye baada ya El Merreikh kujifunga.

Yanga iliongeza bao la pili kupitia kwa Kenneth Asamoah katika dakika ya 37 baada ya kuunganisha krosi ya beki wa kushoto Oscar Joshua.

El Merreikh ilisawazisha bao hilo katikati ya kipindi cha pili na mabao hayo yalidumu hadi mwisho wa mchezo.

Wachezaji walioiwakilisha Yanga leo: Berko, Taita, Oscar, Chacha, Nadir, Gumbo, Mrope, Nurdin, Mwape, Tegete/Asamoah, Kiggi.

4 comments:

Anonymous said...

mambo magumu au vipi?

Anonymous said...

MCHEZO kati ya Yanga na Elman Fc ya Somalia hivi sasa ni mapumziko, Yanga ikiwa mbele kwa bao moja lilowekwa kimiani ya nyota wa kimataifa wa Zambia Davis Mwape katika dakika ya 27

Anonymous said...

vipi mchezo wa kwanza/

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___