Sunday, July 10, 2011

KAGAME CASTLE CUP

Fainali ya kufa mtu

Hatimaye fainali ya Kagame Castle cup ambayo ilikuwa ikisubiriwa na wengi inapigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kati ya Yanga na Simba.

Timu zote mbili zimeingia fainali baada ya kuvuka hatua ya nusu fainali kwa njia ya matuta. Simba iliitoa El Mereikh ya Sudan wakati Yanga iliitoa St. George ya Ethiopia.

Timu hizo mbili zinaingia zikitaka kulinda rekodi zake katika michuano hiyo:

YANGA:
Kocha Sam Timbe katika mechi zote tatu alizotinga fainali. Amefanya hivyo akiwa na SC Villa, Polisi za Uganda na Atraco ya Rwanda.

SIMBA:
Haijapoteza fainali yeyote ya Kagame iliyopigwa katika ardhi ya Tanzania. Tayari imefanya hivyo mara sita.

Mchezaji kwa uhakika atakosa mchezo wa leo kutokana na kadi ni Jerry Santo wa Simba ambaye ana kadi mbili za njano.

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia dola za Kimarekani 30,000

12 comments:

Anonymous said...

haya lete ukweli leo,sio kuogopana.kama wewe simba umekuja hapa karibu lakini ukweli.

Anonymous said...

Mimi ni Yanga, nawapa nafasi kubwa Simba/

Anonymous said...

kikosi cha Yanga leo:
1. Berko
2. Nsajigwa
3. Joshua
4. Chacha
5. Nadir
6. Nurdin
7. Taita
8. Seif
9. Mwape
10. Tegete
11. Kiiza

dakika 30 sasa bado ni 0-0

Anonymous said...

kikosi cha Yanga leo:
1. Berko
2. Nsajigwa
3. Joshua
4. Chacha
5. Nadir
6. Nurdin
7. Taita
8. Seif
9. Mwape
10. Tegete
11. Kiiza

dakika 30 sasa bado ni 0-0

Anonymous said...

leteni matokeo mlio uwanjani

Anonymous said...

dakika 108 gumbo amtungua kaseja mpra bado unaendelea

Anonymous said...

eti huo mpira utaisha saa ngapi? naomba unijibu mdau.

Anonymous said...

samahani ni asamoh kwa kichwa soma ktk blg michuzi.yanga damu kuwait

Anonymous said...

hongera wana yanga kwa ubingwa wa kagame kila la kheri tunangoja maendeleo ziada mkereketwa wa yanga kuwait

Anonymous said...

hayawi hayawi sasa yamekua mnyama kafa na mazishi uwanjani

Anonymous said...

MNYAMA KACHINJWA NA MTU ALIOTOKA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU YAAAAAAAAAAANGA

karawang2 said...

article is very good,
note my adiratna
Adiratna Blog
blog purno