Showing posts with label BURIANI SAID MWAMBA 'KIZOTA'. Show all posts
Showing posts with label BURIANI SAID MWAMBA 'KIZOTA'. Show all posts

Tuesday, February 13, 2007

Buriani Said Mwamba "Kizota"
Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga, Said Mwamba 'Kizota"(41) amefariki dunia juzi usiku baada ya kugongwa na basi la 'daladala'.

Marehemu alikuwa akitoka mpirani kuona mechi ya Simba na Textile de Pungue kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Marehemu ambaye ameacha mjane na mtoto mmoja, alijiunga na Yanga mwaka 1988 akitokea timu ya Tindo ya Tabora.

Mungu ailaze mahala pema roho ya Said Mwamba 'Kizota'