Wednesday, October 03, 2007

TANGAZO:
WANAOTAKA UANACHAMA YANGA

Klabu yenu ya Yanga hivi sasa iko kwenye mchakato wa maaandalizi ya uingizaji wa wanachama wapya.

Katika mchakato huo, tayari fomu zitakazotumika kwa ajili ya maombi ya uanachama zimekwishachapishwa na wakati wowote taratibu zitakapokamilika zitaanza kutolewa nchi nzima.

Kama katiba yetu inavyotaka kwamba mtu yeyote anayetaka kuwa mwanachama ni sharti apitie katika tawi la Yanga sehemu aliko ndivyo itakavyokuwa.

Ni sharti la kikatiba ambalo halipaswi kuvunjwa kwamba wote watakaohitaji kuwa wanachama wa Yanga lazima wapitie katika matawi hayo, kamati za matawi zitawajadili kabla ya fomu hizo kuletwa kwa kamati Kamati Kuu ya Yanga kwa uthibitisho wa kutunuku uanachama.

Tumeona umuhimu wa kutoa ufafanuzi wa jambo hili kutokana na maswali mengi yanayoulizwa na wapenzi wengi nchi nzima juu ya utaratibu gani wautumie ili wawe wanachama wa Yanga.

Tunaomba muwe na subira, utaratibu unaandaliwa utakaomwezesha kila mpenzi wa Yanga anayehitaji kuwa mwanachama apate kadi.

Siku, wiki na mwezi wa kuanza zoezi hili tutawatangazia kupitia vyombo vya habari.

Tunawatakia subira njema.

(imetolewa na uongozi wa Yanga kupitia gazeti lake la Yanga Imara)

1 comment:

Anonymous said...

Huu utaratibu unaoandaliwa utawahusu na wapenzi (wanachama watarajiwa) walio nje ya nchi? Na wale wa mikoani?

Kuwa mwanachama kupitia tawini kuna umuhimu wake naamini, lakini nadhani uanachama wa timu ya mpira (michezo kwa ujumla) hautakiwi kuwa mgumu kuupata. Otherwise, tutawakosa wanachama wasioweza kufuatilia bureaucracy! Watu siku wana mambo mengi mno ya kufanya, kwa hiyo mtu akienda kwenye tawi mara mbili anakuta mwenye kitabu cha kuandika wanachama 'ametoka kidogo', ataondoka moja kwa moja.

Hata uanachama wa CCM ambao zamani ilikuwa lazima uusomee darasa, siku hizi unapatikana kwenye mkutano wa hadhara.

Nadhani (kwa mtazamo wangu) wanachama wapya wangeruhusiwa kuomba unachama popote (makao makuu, kwenye matawi, via email/web?, etc). Mtu akishatimiza masharti ya kulipa ada na kupewa uanachama ndo aambiwe tawi lake la karibu lilipo ili ashiriki pale.

Ushiriki kwenye tawi uwe muhumu / lazima pale mtu anapotaka kugombea uongozi tawini, kwa mfano.

JM.