Tuesday, March 10, 2009

Tumerudi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga imewatandika mabingwa wa soka ligi daraja la kwanza Canada Vancouver White Caps kwa mabao 3-0 katika mchezo wa kujipima nguvu uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Mabao ya Yanga katika mechi hiyo yalifungwa na Jerry Tegete (2) na Mike Baraza.

Ndugu wadau kwa siku kadhaa nimeshindwa kupachika post kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu. Najua ni wengi mtakuwa mmesononeshwa na ukimya huu lakini si nia yangu kufanya hivyo lakini ki-ubinadamu naomba tusameheane na tuendelee na mambo yetu ya kuhabarishana na kubadilishana mawazo kuhusu mambo mbali mbali yanayohusu klabu ya Yanga na wakati mwingine ki-uzalendo tunaizungumzia timu yetu ya Taifa - Taifa Stars.

Amani iwe kwenu.

3 comments:

Anonymous said...

Tuko pamoja

Anonymous said...

Asante bwana CM tulijiuliza ku nani.Tunashukuru kurudi tena.

Anonymous said...

Utapotea tena kesho jioni.5 BILA HAKUTAKALIKA HAPA.KWA WAARABU NYIE ASUSA TU MTAACHIA TU.