Yanga vs Sofapaka
Fainali ya michuano ya Tusker Challenge Cup 2009 inatarajiwa kupigwa jijini Dar kwa Yanga kupambana na mabingwa wa Kenya Sofapaka.
Sofapaka - (SOte kama FAmilia kwa PAmoja Kufikia Azimio) hadi kufikia fainali imeifunga Mtibwa 3-1, imetoka sare na Simba 1-1 na kushinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Tusker FC 4-0.
Yanga kwa upande wake kufikia fainali imezifunga Mafunzo 6-0, Tusker FC 3-1 na kushinda mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba 2-1.
21 comments:
mpira ni mapumziko hivi sasa.
Tupo nyuma kwa 1-0 lililofungwa dk ya 38 kwa freekick.
bado mapema nafasi ya kurudisha na kushinda ipo iwapo mchezo utakuwa kama walivyocheza na mnyama
ni paka hawa wakali naona tukiwadharau watatutoa nishai.wanapiga mpira
ni paka hawa wakali naona tukiwadharau watatutoa nishai.wanapiga mpira
inamaana leo hatuonani kama ck ya mnyama? tuko mbali kaka toa rada
dk 85 tumesawazisha kupitia kwa Boniface Ambani.
Sofapaka muda wote wa 2nd half wamekuwa wakijihami.
nawatakia kila la kheri wana yanga kombe jangwani
dakika ya 90
Tumepata bao la pili kupitia kwa Mrisho Ngassa
Tunaongoza 2-1
Big up all young africans
nilikwambieni dawa yao hao ni samaki kaka asante sana cm yamekua
YANGA IMETWAA UBINGWA WA KOMBE LA TUSKER 2009.
YANGA 2 SOFAPAKA 1
Ahsante sana CM kwa juhudi zako pia hongera kwa ushindi huu kwa wana yanga wooooooote naomba mungu kiwango kizidi ktk raundi ya pili ubingwa jangwani inshaallah
oh! paka! limeshindwa simba jizee ndio paka?
YANGA ndio kiboko ya vijinyama vya mwituni kama paka shume ,simba alozeeka , nk. asante sana shukrani kwa wote waliowezesha. jangwani sasa bardiiiii
Hongereni Wanayanga wote kwa ushindi huo.Yanga sasa iko juu.
Edwardsikawa na CM na wengine wote pia nawatakia mwaka mpya mwema kwa kazi nzuri mliyokuwa mnaifanya mwaka mzima kwa kutupa taarifa muhimu za klabu yetu.Mwenyezi awape nguvu zaidi.
Yanga juu!!!
raha sana!!!
mdau USA.
Yanga Daima Mbele nyuma mwiko
hongera wana yanga wote mdau cuba
Kitendo cha Simba kutoleta wachezaji kuchukua medali zao ni cha kiungwana? Taratibu zinasemaje?
Taratibu gani unauliza..hakuna kitu kama hicho kwenye katiba ya kombe la tusker inayotaka timu ilete wachezaji..Mechi ingechezwa siku hiyo hiyo ya fainali then wachezaji ingebidi wabaki uwanjanai...upoo
anony wa Dec 29, 2009 12:05:00
sasa unaleta za sungura kwamba 'sizitaki mbichi hizi...' hahahaha chako ni chako tu haka kama ni mav*
mnamsusia nani? subirini mwakani muanze upya
Post a Comment