Yanga vs FC Lupopo
Safari ya wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika - Yanga inaanza leo kwa kupambana na timu ya FC Saint Eloi Lupopo ya DRC kwenye uwanja wa Taifa Dar.
Yanga inatakiwa ishinde mchezo wa leo ili kujiweka katika mazingira katika mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Lubumbashi wiki mbili zijazo.
Mchezaji pekee ambaye ni majeruhi kwa upande wa Yanga ni winga Kabongo Honore ambaye alifanyiwa upasuaji wa goti mwanzoni mwa mwaka huu.
Kocha Kostadin Papic anatarajiwa kuteremsha kikosi chake kamili ambacho kimefanya vizuri katika mechi zake tano za mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom. Papic alifunga safari hadi Lubumbashi mwishoni mwa wiki iliyopita ili kusoma mfumo wa uchezaji wa timu hiyo ya DRC.
Kwa upande wao FC Lupopo wanadai wameisoma vizuri Yanga na walituma wawakilishi wao kuja kutazama mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa 3-1.
Tusubiri dakika 90 na kama kawaida tutafahamishana kinachoendelea kutoka uwanja wa Taifa.
60 comments:
MWANA USIJISAHAU KUTUPA MATOKEO
Yanga wanapata bao la kwanza kupitia kwa Ambani katika dakika ya 5 tu. Lete raha wana wa Jangwani!!
nipo uwanjani sasa. Mpira bado haujaanza
Line up:
1. Berko
2. Nsajigwa
3. Maftah
4. Wisdom
5. Nadir
6. Chuji
7. Nurdin
8. Abdi
9. Ambani
10. Ngasa
11. Kiggi
dakika ya 3 tumelambwa bao 1
dakika ya 3 tumelambwa bao 1
yanga amefungwa tatu mpaka half time
Simba wanawashangilia sana hawa jamaa
FAN
it is still the first half and result not yet known don't get tense with what people are posting,CM will give u full updates.
Jamani acheni kutudanganya hebu tuambieni ukweli, cc tunawategemea nyie huko kutupa habari. Kwanza kama mech itaanza saa 10 hii ina maana kuwa half time haijafika.
Mabeki wanakatika sana...
FAN
CM tu ndie wa kuaminiwa. Keep up your good work CM
Ni kweli kabisa ndugu yangu CM ndiyo repoter wetu uwanjani na pekee ndiye tunayemwamini. shukrani sana CM kwa mchango wako huo, wewe ndio ulitakiwa upewe hii website uimantaine maana kwa ku-update tu uko NO1. Big number.
DK 21 bado 0-1.
FAN
Tumefungwa la pili dk ya 38
FAN
Mfungaji Pjilip Marufu
Simba wanawashangilia sana! Beki leo inatuangusha sana..
FAN
mpira halftime bao ni zilezile 0-2
FAN
cm vipi tunangoja ukweli kutoka kwako hawa simba wanaingia na kutupandisha presha
halftime 0-2.
Jamaa ni wazuri mno kwenye kupanga mashambulizi.
Mtandao unasumbua sana hapa uwanjani.
halftime 0-2.
Jamaa ni wazuri mno kwenye kupanga mashambulizi.
Mtandao unasumbua sana hapa uwanjani.
Tegete ameingia. kipindi cha pili kimeanza sasa.
FAN
msiwe na presha sisi tunaweka ukweli humu.mpira mkubali leo mpira umewashinda.mabeki wenu wote wanaharisha leo na makamasi mpaka mdomoni.naona madenga na manji wanaingia badala ya ngasa na chuji.
ambani na Abdi wametoka huku nafasi zao zikichukuliwa na Tegete nna Bonny
Jamani kuna natumaini yoyote? Au ndio tubaki kuwa watalaam wa ligi yetu ya nyumbani? Yaani pamoja na majigambo yote ya Madega timu inaadhirika hivi? Papic anafanya nini?
Dk ya 6 Tumepata bao moja mfungaji ni Kigi Makassy. Afadhali sasa.
FAN
kiggi Makassy anaipatia Yanga bao
Ni 1-2 dakika ya 50
Bao ni 1-2 sasa.
FAN
Tunashambulia sasa..vijana wameamka..
FAN
Dk ya 60 bado 1-2. Bengo anapasha Misuli.
FAN
Tumerudisha 2-2
FAN
sasa nyie hata kupasha misuli mnaandika mnatutia presha jamaa sisi tupo nje ya bongo hamjui tunaufatilizia vipi mpira huu
dk 24 Mrisho Ngassa anafunga bao.
FAN
Simba wako kimya sasa...
FAN
2-2 Ngassa
wanga hao na wakae kimya wanafaida gani
DK 30 bado 2-2
FAN
tumefungwa bao la tatu
Ndhlovumania
Tumefungwa la tatu. Bao ni 2-3 Dk ya 37. Uzembe wa mabeki tena wanajisahau sana!
Tumefungwa la tatu. Bao ni 2-3 Dk ya 37. Uzembe wa mabeki tena wanajisahau sana!
simba wanashangilia tena
Tumepigwa chuma cha nne
kwa sisi wenye roho nyepesi tunaondoka uwanjani
Dk za majeruhi sasa.
FAN
Jamaa kwa kweli wana uwezo mkubwa.
FAN
Bao ni zile zile 2-3.
FAN
Mwanangu kazi tunayo kusonga mbele kwenye mashindano .. haya jamaa ni wazuri mnoo,
hata hao simba wengeondoka wengekua wao
Mpira umekwisha tumelala 2-3.
Mabeki tunalia nao, hawakuwa makini..
FAN
FT 2-3
goodbye to champion leaque maybe 2012.hahaha.mnatia aibu.labda mngecheza nao uwanja wa kaunda.
goodbye to champion leaque maybe 2012.hahaha.mnatia aibu.labda mngecheza nao uwanja wa kaunda.
Ama kweli ng'ombe wa maskini hazai. Pamoja na full mkoko wa wageni, msaada wa maana toka kwa Manji lakini bado yeboyebo mdebwedo!! sasa mnataka msaidiwe vipi nyie?
Labda mpaka wasaidiwe na Rais JK ambae naye anaona aibu timu inavyo boa.nendeni mkajifariji na hiyo kombe ya ulevi mliyoshinda baada ya kubebwa.hakuna kitu timu imejaa uozo tupu.
simba mnafanya nini humu watani acheni wivu anzisheni blog yenu especially wale wanao-post habari za uongo hata kama mtani kama unaweka vitu vyo uongo haipendezi sio ustaarabu.
Jamaani kuna haja ya sie wenye mawazo pevu kuamka na kuibadili klabu yetu.
Kifupi jana tulicheza mpaka mwisho wa uwezo wetu ukiacha huo CM aliouita ugonjwa wa Ndlovumania.
Ok we now have a competent coach at our club, but personally I’m not happy with the way we run our team especially our future plans.
We have to bank on youth technical development, something which we don’t have at the moment.
Ukiangalia vizuri unagundua kuwa wachezaji wetu wengi hawana professional skills za kuweza kumudu soka la kisasa, na hizi wachezaji wanafundishwa kwenye academies.
SWALI la msingi,
KITU GANI KINAKWAMISHA YANGA KUTOKUWA NA ACADEMY YAKE ILIHALI JENGO LA KUKAA LIPO?
Tulisema sana wakati wa mashindano ya ligi ya U-20 ambapo katimu ketu walikuwa wanaokotana saa moja kabla ya mechi na wakaishia kufungwa kwa aibu.
Jambo jingine tuanze muda huu kuscout wachezaji wazuri wa kuwasajili mwakani ili wachukue nafasi za waliochoka.
Hili litatusaidia kuepuka usajili kama wa kina JAMA MBAA(MADEGA)
Yanga bwana hawana akili za mpira wa mashindano ya kimataifa. Wamezoea vikombe vidogo vidogo na ligi za ndani kwa msaada wa marefarii, ila wakikanyaga tu kwy anga za kimataifa ni kichapo. Kocha wenu kwa wiki nzima alikuwa akijigamba mpaka akaenda DRC kuwapeleleza, mpira hauko hivyo angalia vilabu km Man U au chelsea kila siku wanacheza na mechi zao zinaonyeshwa laivu, lkn huwezi kuwasoma na hawatabiriki na ukitiia mguu tu ni kichapo. nyinyi mumekataza eti mechi zenu za Ligi zisionyeshwe na ITV kisa wapinzani wenu watawasoma, mambo ya kizamani hayo inabidi mubadiike! Yebo yebo Mdebwedo! Kudadeki
wewe smba kalale mbele mdebwedo mama na baba yako koma kabisa kutuingilia simba tafathari kaoshe vyoo vya city
na wewe tina unatafuta bwana hakuna bwana hii ni jili ya nyanga 2 atununui mademu pole sana nenda msimbazi
mnaringa bure hakuna kitu.timu yenu mbovu.walipeni mshahara wachezaji wenu wanalia njaa wanasubiri hela ya mwezi wa januari.sijui mtafika aje DRC Congo.
Yanga haina tatizo la pesa hiyo ni furahisha kijiwe ya mapaparazi.
Post a Comment