Saturday, October 16, 2010

Simba achinjwa Mwanza
Bao pekee liliofungwa na Jerry Tegete katika dakika ya 71 limetosha kuipa timu ya Yanga ushindi wa 1-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom ulioisha hivi punde.

Tegete alianza siku ya leo kwa kuacha ujumbe kwenye facebook "Huu wa leo kama ni mziki basi segere huku yanga huku simba ngoma ipo kati mpaka kieleweke!! Gudmrn' friends n' siku njema wish us luck pls!" bila shaka alijua kwamba leo itakuwa siku ya pekee kwake.

Hongera wana Jangwani.

4 comments:

Anonymous said...

Safi sana! Hongera Yanga.

Unknown said...

Naona wale jamaa zetu wenye tambo na vuvuzela nyingi wameacha kusoma blog yetu. Kwani walikuwa wanachonga sana. Sasa wametulia kama maji mtungini. Tegete Noma!!!

Anonymous said...

kwa ujumla hawana jipya. wamebaki kuishia kusema kwenye magazeti. ubingwa kwa mwaka huu mungu atajaalia. we fikiria kocha amekuwa kama mtu wa day pay!

Anonymous said...

Mnasemaje sasa watani.droo 3 mfululizo.kukubali mlibahatisha hata papic alikubali simba ilicheza vizuri.haya tunawacha ndugu zangu.pwenti 2 tuko juu.indeketa hiyo! Beeb beeb