Tuesday, December 21, 2010

Kombe la Shirikisho Afrika 2011

Yanga kuanza na Wahabeshi


Shirikisho la soka barani Afrika limetoa ratiba ya michuano yake ya vilabu kwa mwaka 2011.

Katika ratiba hiyo, Yanga imepangiwa kuanza katika raundi ya awali dhidi ya klabu ya Dedebit ya Ethiopia na kisha kuwafuata Wahabeshi hao wiki mbili baadaye. Mchezo wa kwanza utapigwa kati ya Januari 28.29 na 30.

Endapo Yanga itavuka kikwazo hicho, itabidi isafiri hadi Misri kupambana na Haras El Hadood katika raundi ya kwanza.

Habari ndiyo hiyo.

7 comments:

Anonymous said...

nie vunjeni klabu ya mpira muunde klabu ya taarabu,manaake hamuelewi jinsi ya kuendesha soka.wapenzi wote wasusie michezo yenu sijuui itakuaje.

Anonymous said...

haya sasa tumenunua mbuzi kwenye gunia leupe (mwape)si unaona ndiyo maana wachezaji wanadai zao,haya papic sijui unaonaje hili issue au unategemea utapata ukocha kenya?

Anonymous said...

Acheni hizo!! Si mlikuwa mnajisifu kuwa mna hela? N bado Mabuzi mengi tu meeeeeee!!!

Anonymous said...

ukweli Yanga hatuna viongozi sahihi! maana ni mambo ya aibu mnayotufanyia. katika hali ya kawaida iweje hakuna taarifa sahihi kutoka kwa Uongozi kwa haya yanayofanyika>! mnatutia aibu!

Anonymous said...

ebu tujulisheni hii habari ya minziro kujiunga na kambi ya yanga znz,ina maana papic byebye?

Anonymous said...

hakuna viongozi wenye hekima na busara hizo hela za mishahara itatoka wapi?tunamlaumu manji kweli hiyo ni haki? manji alikua anasema jamani yanga aamkeeni tukadhani anatania ,sasa haya aibu tupuu.

Anonymous said...

tatizo sio kocha tumezoea kubebwa sasa mbebeo imekatika bla blaaa nyingi kama kawaida yetu kandambili eti tunatafuta viongozi angalau wamefuta ujinga , pambafuuuu. bora asie soma mwenye maarifa ya kuendesha kazi zake kuliko fom 4 mitope. ovyoooo!!!! mnasajili kwa bei mbaya halafu hao watu hawaisaidii timu, kichefu chefu mtupu ,

TUACHIENI YANGA YETU, TIMU IMEVAMIWA NA MIJITU YA KUJA MATOKEO NDIO HAYO KILA MTU ANATAKA JINA KUPITIA YANGA SIO KULETA MAENDELEO.

mdau nchi za watu