Wednesday, March 30, 2011

Ligi Kuu ya Vodacom

Yanga 2 Azam FC 1
Mbio za kuelekea katika ubingwa wa ligi kuu ya soka ya Vodacom imezidi kunoga baada ya Yanga kuichapa Azam FC 2-1.

Ushindi huo unaifanya Yanga kujikusanyia pointi 43 ikiwa ni pointi 2 tu nyuma ya Simba yenye pointi 45. Timu zote zimebakiza michezo miwili.

Katika mchezo wa leo uliopigwa kwenye uwanja wa Uhuru, Azam ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 4 kupitia kwa John Boko.

Yanga ilisawazisha katika dakika ya 42 na kuongeza bao jingine katika dakika ya 68 yote yakiwa yamefungwa na Jerry Tegete.

4 comments:

Anonymous said...

Yanga 0 African Lyon 1

Anonymous said...

aisee we bwana acha tuuuu,yanga ni moto utasikia

Anonymous said...

Kipindi cha Pili kimeanza African Lyon wapo mbele kwa goli 1

Anonymous said...

Yanga 3 African Lyon 1